1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz auonya upinzani dhidi ya suala la uhamiaji

30 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameutuhumu upinzani wa siasa za wastani za mrengo wa kulia kwa kutaka kuchukua misimamo mikali kuelekea suala la uhamiaji.

SPD | Olaf Scholz
Kansela wa ujerumani Olaf Scholz ameonya juu ya mwelekeo wa upinzani kuelekea suala la uhamiajiPicha: Michael Kappeler/dpa/picture-alliance

Suala la uhamiaji linatarajiwa kuchukua nafasi na ushawishi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu, mwaka ujao.

Scholz amesema kwenye mkutano wa kampeni hii leo kwamba upande wa upinzani wa vyama vya CDU/CSU unatishia kubadilisha sera ya sasa kwa sababu hautaki kukubaliana na uhalisia.

Amewaambia wawakilishi karibu 500 wa chama hicho katika makao makuu ya chama mjini Berlin kwamba Ujerumani kwa muda mrefu imekuwa ikiwategemea wahamiaji, akiwaangazia karibu wakazi milioni 25 wenye asili ya uhamiaji.

Ujerumani inataraji kufanya uchaguzi Februari 23 kufuatia kura ya imani ya bunge ya mwezi Disemba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW