Kansela Scholz ataka Ujerumani iwe na mifumo ya kujilinda
8 Desemba 2022Matangazo
Katika mahojiano yaliyochapishwa leo na shirika la habari la Funke na gazeti la Ufaransa la Ouest, Scholz amesema serikali yake kwa sasa inafanya mazungumzo na watengenezaji wa mifumo hiyo mbalimbali ili kujiweka tayari kufanya maamuzi.
Kansela huyo wa Ujerumani vile vile amesisitiza lengo lake la kuongeza matumizi ya ulinzi ya Ujerumani ili kufikia lengo la asilimia mbili ya pato jumla lililowekwa na wanachama wa Jumuiya Kujihami ya NATO.
Ujerumani na zaidi ya washirika wake 12 wa NATO wanalenga kununua kwa pamoja mifumo ya kujilinda angani inayoyalinda maeneo ya nchi jirani kutokana na makombora.