1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz atetea mipango ya pensheni katika bajeti 2025

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametetea mipango ya serikali yake kuhusu pensheni katika mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2025.

Ujerumani | Kansela Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Katika mjadala uliofanyika bungeni jana, Kansela Scholz alisema kwamba serikali yake ina mipango mikubwa kuhusu uhakika wa viwango vya pensheni.

Kwa upande wake kiongozi wa upinzani wa chama cha mrengo wa wastani kulia cha CDU, Friedrich Merz ameishambulia bajeti hiyo na kuituhumu serikali ya Scholz kwa kuharibu soko huria. 

Soma pia:Ujerumani yasema bajeti finyu haitawazuia kuisaidia Ukraine

Merz amedai kuwa muungano wa Scholz umeifanya sera ya kijamii kuwa mzigo kwa kizazi kichanga ambacho kitalazimika kulipa mafao zaidi. 

Kiongozi huyo wa upinzani amesema kila uamuzi unaofanywa na serikali ya Kansela Scholz umezidisha hali ya ushindani kwa uchumi wa Ujerumani. Scholz ametoa utetezi huo wakati waziri wake wa ulinzi akikabiliwa na maswali magumu juu ya ufadhili wa jeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW