1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz atetea sera ya serikali yake kuhusu uhamiaji

11 Septemba 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani ametetea sera ya serikali yake, kuhusu uhamiaji mbele ya bunge mjini Berlin leo na kusisitiza kwamba nchi hiyo inahitaji kuvutia wafanyakazi wa kigeni wenye ujuzi.

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani Picha: John Macdougall/AFP/Getty Images

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani ametetea sera ya serikali yake, kuhusu uhamiaji mbele ya bunge mjini Berlin leo na kusisitiza kwamba nchi hiyo inahitaji kuvutia wafanyakazi wa kigeni wenye ujuzi.

Kansela Scholzamesema hakuna nchi duniani yenye idadi ndogo ya wakaazi inayoweza kuwa na ukuaji wa kiuchumi na huo ndio ukweli unaoikabili Ujerumani kwa sasa. Matamshi hayo ya Kansela, ameyatowa  katika kiwingu cha mvutano na mjadala mkali uliopamba moto bungeni kuhusiana na suala la sera ya uhamiaji na waomba hifadhi.

"Uongozi sio kupanda kiunzi na kutowa mapendekezo ya lazima kwa kuonesha ubabe .Uongozi ni kubadilisha mambo na kuwa na uwezo wa kuwashawishi watu wako kufikia mwafaka wa pamoja. Huo ndio uongozi bwana Friedrich Merz.''

Kiongozi huyo wa Ujerumani amemkosoa kiongozi wa upinzani wa chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia cha Christian Democratic Union, CDU Friedrich Merz, akisema anaupa nguvu upande wa siasa kali za mrengo wa kulia, kwa kukataa kuingia kwenye mazungumzo ya nia njema kuhusu mabadiliko ya kweli ya kisera.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW