1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz atoa heshima kwa vyama vya wafanyakazi

29 Aprili 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa ujumbe wa kuonesha heshima kwa vyama vya wafanyakazi nchini mwake, muda mfupi kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani-Mei Mosi

Bundeskanzler besucht die Berliner Verkehrsbetriebe
Picha: Kay Nietfeld/picture alliance/dpa

Ameutoa ujumbe huo kufuatia mfululizo wa migomo ambayo imevuruga uchumi wa taifa hilo. Katika ujumbe wake kwa njia ya vidio kansela huyo amesema kipindi hiki heshima ya wafanyakazi lazima iwe kiini cha kila demokrasia.

Soma zaidi:Serikali ya Ujerumani yakubali kuongeza mishahara

Akizungumza kama mwanachama wa chama cha wafanyakazi na wakili wa zamani wa wafanyakazi, alivisifu vyama vya wafanyakazi kwa kujitolea kwao kwa ustawi haki za serikali na wafanyakazi.

Tangu kuanza kwa mwaka huu raia wa Ujerumani wamekuwa wakikabiliwa na athari za migomo mingi ya wafanyakazi wa huduma za umma na wa usafiri wa umma kuhusu malipo na mazingira duni.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW