Kansela wa Austria ziarani Ujerumani
18 Januari 2018Tukianza na mada kuhusu ziara ya kansela wa Austria nchini Ujerumani , mhariri wa gazeti la Berliner Zeitung anaandika.
Muungano wa serikali wa rangi nyeusi na buluu kama unavyoitwa nchini Austria hadi sasa ni wa aina ya mfano barani Ulaya, ambapo vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia vimepata mafanikio makubwa kila mahali na kwamba wakati huu ama baadaye vitaweza kuwa sehemu ya serikali. Gharama ya mafanikio haya, lakini ni kwamba kansela Sebastian Kurz anaweza kukibana chama ambacho hakipendi wahamiaji katika Ulaya cha FPO. Na hili pia lina matatizo yake, na huenda hivi karibuni yakaonekana, hususan wakati Austria itakapochukua uongozi wa Umoja wa Ulaya katikati ya mwaka huu. Miongo kadhaa ya kuwa na mahusiano ya karibu na Ujerumani imepita. Kansela Kurz wa Austria anatafuta sasa washirika wapya katika Ulaya.
Kuhusu mada hiyo hiyo Gazeti la Badische Neueste Nachrichten la mjini Karlsruhe linaandika:
Kansela Angela Merkel mwenye matatizo hawezi kufurahia , kwamba kijana kutoka mjini Vienna atakuwa ni mada ya kujadiliwa hapo baadaye. Hususan katika suala la sera za wakimbizi, suala ambalo kansela Kurz tayari kama waziri wa mambo ya kigeni analidhihirisha, na ni suala ambalo litahitaji kuidhinishwa. Na hata katika kiwango cha Ulaya itabidi kupambana na kansela Kurz , kwa kuwa madai yake, hayaishii tu katika mipaka ya taifa hilo la Austria.
Gazeti la Ludwigsburger Kreiszeitung likizungumzia kuhusu mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto kati ya chama cha CDU / CSU na SPD linaandika.
Muhimu zaidi ni kwamba, mapitio ya hivi sasa kwa pande zote mbili yana uwezekano mkubwa, kwamba hali bora ya muungano inaweza kufikia mwisho na kuiingiza nchi katika mkwamo mkubwa. Iwapo hali kama hiyo ya dharura itatokea. Bila ya upande mmoja kusababisha vurumai , iwapo kutatokea hali ya kuvunjika kwa muungano huo. Makubaliano hususan kwa upande wa SPD yanaelekea vizuri , na hali ya tahadhari inapaswa pia kuwapo, na sio upande wa chama cha kansela Merkel kuwawekea mbinyo zaidi. Mradi huu pia unapaswa kuwa muafaka kwa wapinzani wengi wasipendelea vyama hivyo kuunda serikali. Pamoja na hayo kansela Merkel pia anaweza kutumia matokeo ya muda huu kutumia busara kujiondoa.
Nae mhariri wa gazeti la Rhine-Neckar - Zeitung kuhusiana na mada hiyo anaandika:
Ni mapema mno kuikumbusha serikali mpya ya chama cha CDU/CSU na SPD kuhusu mazungumzo ya viwango vya mishahara. Ni kama muziki ambao unaelekea kufikia mwisho. Kwa kweli kunaonekana kuwapo na hali ya wasi wasi, iwapo serikali kama hiyo inaweza kutokea. Kwa sababu hali ya mjadala wa muungano wa serikali kati ya chama cha CDU na SPD haupigi hatua.
Mada ya mwisho ni kuhusu Marekani ilivyochukua hatua ya punguza mchango wake katika shirika la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Gazeti la Nordwest-Zeitung la mjini Oldenburg linandika:
Katika mataifa ya Kiarabu hivi sasa kuna ukimya kuhusiana na hali ya wakimbizi wa Kipalestina. Katika Ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi shirika la UNRWA ndio linashughulikia matatizo ya wakimbizi wa Kipalestina. Shirika hili la Umoja wa Mataifa linawajibika kuwahudumia wakimbizi wa vizazi na vizazi. Zaidi ya hayo katika Ukanda wa Gaza UNRWA linawapatia kazi maelfu ya watu wanaounga mkono kundi la Hamas. Katika shule zinazohudumiwa na shirika hilo wanajitokeza wafuasi wa kundi hilo ambao wanachochea chuki dhidi ya Israel. Kwa ujumla mhariri anaandika kwa shirika hilo ni sehemu ya matatizo na sio suluhisho. Ni vizuri kulitaja tatizo kwa jina lake.
Kwa maoni hayo ndio tunafikia mwisho wa kuwaletea uchambuzi wa yale yaliyoandikwa na wahariri wa magazeti hapa Ujerumani , kama mlivyokusanyiwa na Sekione Kitojo.
Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Gakuba, Daniel