1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz aelekea China kwa mazungumzo na Rais Xi Jinping

Amina Abubakar Reuters, AFP
24 Februari 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ametoa wito kwa wafanyabiashara kusisitiza ushindani ulio na usawa katika biashara na China, wakati akielekea Beijing kukutana na rais Xi Jinping.

Deutschland Köln 2025 | Bundeskanzler Friedrich Merz reist zum G20-Gipfel nach Johannesburg
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Wolfgang Niedermark mwanachama wa bodi ya Shirikisho la viwanda vya Ujerumani (BDI) amemtolea wito Merz kushughulikia waziwazi masuala kama vile uwezo kupita kiasi, upotoshaji kwenye ushindani na udhibiti wa mauzo ya nje ya malighafi muhimu.

Amesema ni wazi  kwamba kampuni za Ujerumani na Ulaya haziko tu katika ushindani wa kibiashara na makampuni makubwa ya China lakini pia yapo katika ushindani ya kimifumo iliyoundwa na mataifa tofauti. Niedermark amesema bila ya mabadiliko upande wa China, mivutano mipya ya kibiashara na Umoja wa Ulaya huenda ikatokea.

Amesema udhibiti wa madini adimu ya China yanatishia usalama wakiuchumi wa Ulaya huku taratibu za leseni zisizo wazi na ufikiaji wa soko teule zikipotosha zaidi ushindani na kuathiri maamuzi ya uwekezaji.

Rais wa China Xi Jinping akiwa na Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Li Xueren/Xinhua/-,Yauhen Yerchak/Zuma Wire/picture-alliance

Merz anaondoka leo Jumanne kwenda China kwa ziara yake ya kwanza tangu alipokuwa kansela mwaka uliopita.

Ziara ya Merz itaugusia pia mgogoro wa Urusi na Ukraine

Siku ya Jumatano atakutana na Rais Xi Xinping mjini Beijing na miongoni mwa mambo watakayoyajadili pia ni masuala ya kiusalama ikiwemo mgogoro wa Urusi na Ukraine ambao umeingia mwaka wake wa nne hii leo Februari 24, 2026. Mengine yatakayojadiliwa ni ushirikiano wa kiuchumi wa na China.

Kansela huyo wa Ujerumani pia anatarajiwa kujadili masuala ya haki za binaadamu nakuutembelea mji maarufu wa Forbidden City" huko huko mjini Beijing. Katika ziara yake ya China Merz ameandamana na ujumbe wa biashara na  pia atalitembelea jiji la kibiashara la Hangzhou.

Uchumi wa Ujerumani unaoongozwa na mauzo ya nje, umekuwa ukitegemea zaidi soko kubwa la China katika miaka ya hivi karibuni, lakini pia mauzo ya bidhaa za Ujerumani kama vile magari yamepungua kutokana na ushindani wa ndani unaoongezeka. China ilikuwa mshirika mkuu wa biashara wa Ujerumanimwaka wa 2025, ikiipiku Marekani kutokana na sera za ushuru za Rais Donald Trump.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW