Kansela wa Ujerumani aitembelea Romania
3 Aprili 2023Matangazo
Ziara hiyo pia ni ya kuonesha mshikamano na Moldova ambayo ni jirani wa Romania na ambayo inaonekana hasa kuwa katika nafasi hatari tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka jana.
Rais wa Moldova Maia Sandu ambaye anaituhumu Moscow kwa kuchochea machafuko katika nchi yake anatarajiwa pia kujiunga na kansela Scholz pamoja na rais wa Romania Klaus Lahannis katika mkutano utakaofanyika baadae mjini Bucharest.
Mazungumzo ya viongozi hao yanatarajiwa kujikita kwenye uchumi,nishati na usalama. Kansela wa Ujerumani ameisifu Romania kwa kwa utayari wake wa kuwapokea wakimbizi wanaomiminika kutoka Ukraine akisema Ujerumani inasimama kwa dhati na Romania.