1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz aelekea India kuimarisha mahusiano ya kibiashara

11 Januari 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anaelekea India hii leo Jumapili wakati kukiwa na changamoto kubwa barani Ulaya ikiwemo kupanda kwa ushuru wa Marekani pamoja na vitisho vya Urusi na China.

Belgien Brüssel 2025 | Friedrich Merz
Knasela wa Ujerumani Friedrich Merz Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Baada ya ziara za viongozi waliopita, sasa Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anatarajiwa kuzuru India kuanzia Januari 11 hadi 13, ambapo atakutana na Waziri Mkuu Narendra Modi katika jimbo la Gujarat na baadaye kuzuru Bangalore kukutana na wawakilishi wa kampuni za Ujerumani.

Ziara hiyo inaambatana na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara, ikionyesha uzito wake wa kiuchumi.

Katika dunia inayozidi kuwa na misukosuko ya kisiasa na kiusalama, Ujerumani inatafuta washirika wapya wa kuaminika, hasa wakati mshirika wake wa jadi, Marekani, ameanza kuchukua hatua zinazotia wasiwasi kama vitisho dhidi ya Greenland na ushuru mkubwa kwa bidhaa za Ulaya.

Ujerumani inaiona India kama mshirika muhimu kwa sababu ya ukuaji wake mkubwa wa kiuchumi (wa zaidi ya asilimia sita), tofauti na Ujerumani inayokabiliwa na mdororo wa uchumi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW