1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kansela Merz kukutana na Trump Ikulu ya Whitehouse

3 Machi 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne. Ziara hiyo ni ya pili ya Kansela Merz nchini humo tangu alipoingia madarakani miezi kumi iliyopita.

Berlin, Ujerumani 2026 | Kansela Friedrich Merz akizungumza na wanahabari mjini Berlin kuhusu hali ya Mashariki ya Kati 01.03.2026
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: dts-Agentur/picture alliance

Mazungumzo hayo yaliyokuwa yamepangwa kabla ya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, yalitazamiwa kujikita katika vita vya Ukraine pamoja na ushirika wa mashaka wa kibiashara kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya.

Ujerumani yajitenga na hatua za Marekani na Israel

Licha ya kuwa Ujerumani haihusiki na mashambulizi dhidi ya Iran, Merz ameeleza kuwa anaelewa hatua za kijeshi zilizochukuliwa na Israel na Marekani lakini hakuzikosoa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW