1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aanza ziara barani Afrika

4 Mei 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameanza ziara yake ya kuu ya pili kuelekea Afrika leo.

Kanzler Scholz beginnt Afrika-Reise
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiabiri ndege kuelekea Ethiopia, kituo cha kwanza cha ziara yake barani Afrika.Picha: picture alliance/dpa

Ziara ya Scholz hiyo italenga juhudi za utatuzi wa migogoro na ulinzi wa amani, tabia nchi, mada kuhusu nishati jadidifu pamoja na madhara ya vita vya Urusi nchini Ukraine.

Scholz anatarajiwa kwanza kutua Ethiopia kwa mazungumzo na serikali ya taifa hilo pamoja na maafisa wa Umoja wa Afrika.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka miwili katika jimbo la Tigray vilisababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu.

Baadaye jioni, Scholz ataelekea Kenya, nchi ambayo ni mshirika muhimu zaidi kwa Ujerumani katika kanda ya Afrika Mashariki.

Kenya imekuwa ikiongoza jukumu muhimu la upatanishi na usuluhishi wa mizozo ya kikanda na tayari imejitolea kushiriki katika juhudi za kupunguza machafuko ya Sudan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW