Scholz anapanga kuzungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin
10 Juni 2023Matangazo
Akihutubia kongamano la kanisa la Kiprotestanti la Ujerumani mjini Nuremberg, Scholz amesema aliwahi kuzungumza na Putin kwa njia ya simu katika siku za nyuma na kwamba anapanga kufanya hivyo tena. Scholz ameongeza kuwa sio busara kuilazimisha Ukraine kuidhinisha na kukubali uvamizi huo wa Urusi na kwamba baadhi ya maeneo yake yageuka ghafla kuwa ya Urusi.
Scholz asema atajitahidi kuona NATO haijumuishwa katika vita
Kansela huyo pia amesema atajitahidi kuona kwamba jumuiya ya kujihami ya NATO haijumuishwi katika vita hivyo. Urusi na Ukraine zote zimeripoti mapigano makali nchini Ukraine hapo jana Ijumaa lakini bado haijabainika wazi iwapo mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Ukraine yaliosubiriwa kwa muda mrefu bado yatafanyika.