1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa Ujerumani azipongeza jumuiya za wafanyakazi

30 Aprili 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amezipongeza jumuiya za wafanyakazi pamoja na wafanyakazi kabla ya kuadhimishwa siku ya wafanyakazi duniani, hapo kesho Mei mosi.

Bundeskanzler besucht die Berliner Verkehrsbetriebe
Picha: Kay Nietfeld/picture alliance/dpa

Scholz amewasilisha pongezi hizo baada ya miezi kadhaa ya harakati zilizosababisha vurumai katika uchumi wa nchi. Kansela wa Ujerumani amesema huu ni wasaa wa kusisitiza kwamba maslahi ya wafanyakazi yanapaswa kuwamo katika moyo wa demokrasia.

Amezipongeza jumuiya za wafanyakazi kwa kuyazingatia maslahi ya kijamii na haki za wafanyakazi. Harakati za hivi karibuni za jumuiya hizo zilizoendeshwa kote nchini Ujerumani, ziliathiri huduma za afya, usafirishaji, posta na huduma kadhaa katika sekta nyingine za uchumi.

Soma pia: Kansela Scholz atoa ujumbe wa heshima kwa vyama vya wafanyakazi

Jumuiya hizo zinapigania malipo zaidi kwa wafanyakazi pamoja na mazingira mazuri ya kazini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW