Kansela wa Ujerumani Scholz apongeza juhudi za amani Ukraine
13 Agosti 2023Matangazo
Katika mahojiano yake ya kila mwaka ya msimu wa kiangazi na televisheni ya Ujerumani ya ZDF, Scholz amesema ni vyema kwa jamii ya kimataifa kuendeleza mazungumzo, kwa sababu yanaongeza mbinyo kwa Urusi kufahamu kuwa imeuchukua mkondo mbaya na kwamba lazima iwaondoe askari wake Ukraine na kutoa nafasi ya kupatikana amani.
Soma pia: Mkutano wa kimataifa juu ya Ukraine wamalizika Jeddah
Wawakilishi kutoka karibu nchi 40 zikiwemo China, Ujerumani, India na Marekani zilishiriki katika mazungumzo ya mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Jeddah, ijapokuwa Urusi haikualikwa. Mazungumzo sawa na hayo ya kimataifa ya kujadili mkondo wa kupatikana amani Ukraine yalifanyika pia mjini Copenhagen, Denmark mwezi Juni.