Kansela wa Ujerumani Scholz kuteuliwa kugombea uchaguzi
22 Novemba 2024Hayo yamesemwa na mwenyekiti mwenza wa cha Social Democratic - SPD. Haya yanajiri baada ya mpinzani wake mkuu ndani ya chama, Waziri wa Ulinzi Boris Pistorius, kukataa kugombea.
Pistorius alisema Scholz ndiye mgombea sahihi wa chama. Pia alisema itatuma ishara mbaya kumvua kansela aliyeko madarakani wadhifa wake. Ujerumani utafanya uchaguzi wa mapema Februari mwakani baada ya serikali ya muungano ya vyama vitatu kusambaratika mwezi uliopita.
Soma pia: Scholz akabiliwa na shinikizo la kumtaka kutogombea tena
Wanachama waandamizi wa chama cha upinzani cha Christian Democratic Union - CDU wamesema kuwa ingawa Scholz huenda ameshinda mapambano ya madaraka ya ndani ya chama, bado hapendwi na wanachama wengi wa chama chake.
Soma pia: Chama cha Kansela Olaf Scholz kinamshinikiza kiongozi huyo kumuachia nafasi Boris Pistorius
Hata hivyo, ikiwa Scholz anataka kuchaguliwa tena, atalazimika kupambana vikali, kwa kuwa SPD kwa sasa iko nyuma sana katika uchunguzi wa maoni. Chama hicho kiko nyuma ya muungano mkuu wa kihafidhina wa CDU/CSU. Pia kiko nyuma ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani AfD.