1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela wa zamani wa Austria Sebastian Kurz atiwa hatiani

24 Februari 2024

Kansela Kurz amepatikana na hatia kwa kutoa ushahidi wa uongo kwa kamati ya bunge iliyokuwa ikichunguza visa vya rushwa katika serikali yake.

Österreich Ex-Kanzler Sebastian Kurz
Kansela wa zamani wa Austria, Sebastian KurzPicha: Lisa Leutner/AP Photo/picture alliance

Mahakama ya mjini Vienna imemkuta na hatia kansela wa zamani wa Austria Sebastian Kurz kwa kosa la kutoa ushahidi wa uongo katika uchunguzi wa bunge na kumuhukumu kifungo cha miezi minane jela kilichosimamishwa.

Hukumu hiyo ya jana Ijumaa ilitolewa mwishoni mwa kesi iliyokuwa ikisikilizwa kwa miezi kadhaa dhidi ya mwanasiasa huyo wa zamani ambaye aliwahi kupongezwa kama mwanasiasa mwenye umri mdogo aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kushangaza miongoni mwa mahafidhina wa Ulaya.

Kurz, mwenye umri wa miaka 37, amesema atakata rufaa akiieleza hukumu dhidi yake kuwa ya kushaganza na isiyo ya haki.

Kurz alihukumiwa kwa kupotosha uchunguzi wa bunge kuhusu kashfa mbalimbali za rushwa ambazo ziliiangusha serikali yake ya kwanza ya mseto na chama cha mrengo mkali wa kulia mnamo 2019.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW