1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Schröder: Magharibi ni lazima izungumze na Putin

28 Machi 2024

Kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schröder anasema mataifa ya Magharibi yanastahili kuketi katika meza ya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa ajili ya kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Maonyesho ya Hannover 2005 | Vladimir Putin na Gerhard Schröder
Kansela wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schröder (R) akiendesha trekta na Rais Vladimir Putin 11.04.2005. Schröder ameyaraia mataifa ya magharibi kuzungumza na Putin ili kumaliza vitaPicha: R. Jensen/dpa/picture-alliance

Katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani dpa, Schröder anadai kwamba urafiki wake na Vladimir Putin unaweza kuchangia katika kuvimaliza vita hivyo.

Uongozi wa chama chake cha Social Democratic Party umemtenga kutokana na hatua yake ya kutomkosoa Rais Putin kutokana na vita hivyo kufikia sasa.

Kwengineko jeshi la Ukraine linasema limezidungua droni 26 kati ya 28 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo.

Jeshi hilo limeongeza kwamba droni hizo zilizotengenezwa nchini Iran, zilidunguliwa katika maeneo ya mashariki, kusini na kusini mashariki mwa Ukraine. Gavana wa eneo la Zaporizhzhia amesema mwanamke mmoja amejeruhiwa.