Kanzela Merkel ahutubia Bunge la Ulaya
14 Februari 2007
Kwa mara ya pili, Kanzela Angela Meerkel wa Ujerumani, akiwa rais wa Umoja wa Ulaya alilihutubia jana Bunge la Ulaya mjini Strassburg.Mbali na kuungamkono wazi haja ya kuilinda hali ya hewa na mazingira,Kanzela aliukodolea macho pia mzozo wa Mashariki ya Kati.
Akiwa amerudi hivi punde tu kutoka Mashariki ya kati,rais huyo wa Umoja wa Ulaya alilitaka bara hilo kuchangia zaidi katika utaratibu mpya wa kusaka amani katika Mashariki ya kati.Mfano bora wa kuigwa hapo ni kule kukomeshwa kwa vita baridi na kuliunganisha tena bara la Ulaya-alsema Kanzela Angela Merkel.Akaongeza,
“kile kilichodhihirika kuwa miujiza ya enzi yetu kitushajiishe kuwa miujiza katika eneo jengine la ulimwengu huu.Kile ambacho wapalestina na waisraeli hawakumudu kukiiona mingo kadhaa –yaani kuishi pamoja kwa amani katika nchi mbili jirani zisiopigana vita,maisha yenye matumaini ya neema,lazima pia kiwe shabaha yetu.Kwavile tumejionea imewezekana kutoka uhasama tumeingia katika amani na urafiki.”
Urais huu wa Ujerumani wa UU unauwakilisha umoja huo pia katika kundi la pande 4 linalopatanisha mzozo wa mashariki ya kati litakaloonana wiki ijayo mjini Berlin.Wakaazi katika Mashariki ya Kati wanatumai kuona umoja wa Ulaya unashika usukani zaidi na unaingiwa na hofu na wasi wasi juu ya mradi wa nguvu za kinuklia wa Iran.
Kanzela Merkel alikwenda Strassburg kwenye Bunge la Ulaya kutokana na hotuba ya kwanza ya spika wa Bunge hilo Hans-Gert Pöttering .Pöttering alisema hata Bunge la Ulaya linapaswa kusdhughulikia mzozo wa mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini:
„Hatutaki mgongano wa ustaarabu, bali tunachotaka ni amani ,uhuru na haki kati ya mataifa yote na dini zote.Kwa shabaha hiyo tunataka kujenga daraja la kimila na kitaalamu kati ya kingo mbili za bahari ya kati.“
Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani, amebadili msimamo wake wa awali kuhusiana na hali ya hewa wa kufikiwa vipimo vya juu zaidi vya kuzuwia m,ivuke inayochafua hali ya hewa vilivyotakiwa na Tume ya Ulaya.
Kama rais wa UU Bibi Angela Merkel amejiweka sasa usoni kabisa mwa wale wanaotetea mazingira safi.Ameungamkono huko Strassbourg mradi wa Tume ya Ulay