KARACHI:45 wafa katika ajali ya ndege
11 Julai 2006Matangazo
Watu 45 wamekufa katika ajali ya ndege iliyotokea nchini Pakistan. Ndege hiyo ya abiria iliangukia katika mashamba ya nafaka muda mfupi tu baada ya kuanza safari.
Watu waliokuwamo ndani ya ndede hiyo ni pamoja na maafisa wa ngazi za juu wa jeshi na wizara ya sheria.
Inatuhumiwa kuwa hitilafu za ufundi ndizo zilizosababisha ajali hiyo.