Mafunzo
Karandinga: Changamoto za Plastiki
2 Februari 2022Matangazo
Mapambano dhidi ya taka za plastiki yanaonekana kuwa ya dharura, wakati mafuriko yanayotokana na utupaji hovyo wa taka na makosa ya wanasiasa yanayoongezeka yanawasumbua watu. Tunaungana na Mama Rosa na watoto wake Kalulu na Gammy, ambao rafiki yao Ananda ana wasiwasi kuhusu kupotea kwa baba yake. Nini kimemtokea? Hadithi hii ya kusisimua inaangazia jinsi wananchi wanavyoweza kuwataka wanasiasa kuchukua hatua na kuendeleza maoni kwa ajili ya mustakabali bora, endelevu na salama. Hadithi hii imeandikwa na James Muhando kutoka Kenya.