1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Maneno ya Chuki, Maneno ya Amani

4 Machi 2020

Wakati mvutano wa kikabila ukiongezeka nchini mwake, June mwandishi habari kijana anaamua kupambana na kuenea kwa kauli za chuki.

DW Crime Fighters Serienmotiv „Our tongue, our land“

Baada ya kurejea Magange akitokea uhamishoni alikoishi kwa miaka kadhaa, Banku Mutumba, mwanasiasa kijana wa upinzani, anachomwa kisu wakati anawasili kwenye uwanja wa ndege. Hili linazusha mvutano wa kikabila kati ya Waderemba, kabila anakotokea na Watiribe ambao wako madarakani na wanaoshikilia uchumi wa nchi. June mwandishi habari kijana ambaye anatokea kwenye makabila yote mawili, anakabiliana na ongezeko la kauli za chuki na amedhamiria kuuokoa uhusiano wake na mchumba wake ambaye ni Mtiribe. Lakini wahalifu waliomshambulia Banku ni kina nani? Je ni kweli rais anahusika kama ambavyo jamii ya Waderemba inadai? Inspekta Opande anapambana na muda kujaribu kufuatilia kesi hii kabla mzozo wa kikabila haujazuka na kugeuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW