1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu watoto 500 wamefariki kutokana na njaa Sudan

23 Agosti 2023

Shirika la kimataifa la hisani la Save the Children limesema takriban watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan.

Sudan
Mkimbizi wa Sudan na mtoto wake aliyekimbilia ChadPicha: Gueipeur Denis Sassou/AFP

Shirika la kimataifa la hisani la Save the Children limesema takriban watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan, wakiwemo watoto zaidi ya 20 katika kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na serikali katika mji mkuu Khartoum, tangu mapigano yalipozuka nchini humo mwezi Aprili.

Shirika la Save the Children pia lilisema kuwa karibu watoto 31,000 wanakosa huduma ya lishe na matibabu ya utapia mlo tangu shirika hilo la misaada kusitisha shughuli zake kwenye vituo 57 vya lishe nchini Sudan.

Mzozo huo wa Sudan umegeuza jiji la Khartoum na maeneo mengine ya mijini kuwa viwanja vya vita. Wakazi wengi wanaishi bila maji na umeme, na mfumo wa huduma za afya nchini humo umekaribia kuporomoka.

Arif Noor, mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Sudan amesema hawakutegemea kuwaona watoto wakifa kwa njaa katika idadi na hali kama hiyo. Noor amesema wameshuhudia watoto wakifa njaa inayoweza kuzuilika kabisa. Amesema idadi ya watoto walioachishwa shule nchini Sudan pia imeongeza.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW