1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMarekani

Karibu watu 1,000 wa kisiwa cha Maui hawajulikani waliko

23 Agosti 2023

Mamlaka za jimbo la Hawaii nchini Marekani zimesema kati ya watu 500 hadi 1,000 bado hawajulikani walipo kiasi wiki mbili tangu moto mkubwa wa nyika ulipouteketeza mji wa kihistoria wa Lahaina kwenye kisiwa cha Maui.

Joe Biden ziarani Hawaii
Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill, walipoutembelea mji wa Lahaina huko Hawaii kutoa pole kwa janga la moto wa nyika.Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Maafisa wa jimbo hilo wanakabiliwa na changamoto za kubaini kwa uhakika idadi ya watu waliopoteza maisha na wale ambao bado wako hai lakini hawajitokeza kujisajili kuwa wamesalimika.

Hadi siku ya Jumatatu, polisi ilisema watu 115 ndiyo wamethibitika kupoteza maisha kwenye mkasa huo wa moto unaotajwa kuwa ndiyo mbaya zaidi nchini Marekani katika kipindi cha karne moja.

Idadi kubwa ya watu ambao hawajulikani waliko imezidisha taharuki kwenye jimbo hilo katika wakati juhudi zinafanywa kuwasaidia manusura na kutambua miili ya wale walioteketea kwa moto.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW