1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu watu 20 wamekufa katika ajali ya barabarani Uganda

4 Mei 2022

Polisi nchini Uganda imesema watu 20 wamekufa baada ya basi la abiria kuanguka katika shamba la majani chai kwenye barabara kuu moja ya magharibi mwa Uganda.

Simbabwe Symbolbild Bus-Unfall
Picha: Jekesai Njikizana/AFP

Polisi imesema karibu saba kati ya wahanga wa ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi ni watoto wadogo. Msemaji wa polisi Vincent Twesigye ameliambia shirika la habari la dpa kuwa basi hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi na kwamba lilikuwa limejaa kupita kiasi.

Hakukuwa na taarifa ya haraka kuhusu chanzo cha ajali hiyo, ambayo ni miongoni mwa ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea Uganda katika miaka ya karibuni.

Basi hilo lilikuwa njiani kutoka mji wa Fort Fortal kuelekea mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Ajali mbaya kabisa za barabarani hutokea mara kwa mara Uganda, ambako barabara ni nyembamba na zimejaa mashimo. Matukio ya magari makubwa kugongana ana kwa ana ni ya kawaida nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW