SiasaSomalia
Karibu watu 20 wauawa Somalia
2 Januari 2023Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa daktari katika hospitali ya umma.
Mohamed Farah, daktari katika hospitali ya umma ya Laascaanood, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa takriban watu wengine kadha wamejeruhiwa. Amesema ameiona miili ya waliofariki iliopelekwa katika hospitali hiyo.
Waandamanaji wanaitaka Somaliland kuacha udhibiti wa mji huo na pia wamevishtumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kumaliza visa vya ukosefu wa usalama katika mji huo.
Kwa zaidi ya wiki moja, vikosi vya usalama vimekuwa vikipambana na waandamanaji huko Laascaanood, mji wa mashariki mwa Somaliland ambao unagombaniwa kati ya mamlaka ya Somaliland na jirani yake Puntland, mojawapo ya mikoa yenye mamlaka yake ya ndani.