1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Karibu watu 27 wafa maji baada ya boti kuzama, Nigeria

30 Novemba 2024

Karibu watu 27 wamekufa baada ya boti kuzama katika Mto Niger, katikati mwa Nigeria, idara za dharura zimesema jana Ijumaa.

Nigeria , Mto Niger
Sehemu ya Mto Niger nchini Nigeria, ambako watu karibu 27 wamekufa baada ya boti yao kuzama Novemba 28, 2024Picha: Patrick Meinhard/AFP/Getty Images

Msemaji wa Idara inyosimamia masuala ya dharura kwenye jimbo la Kogi, Sandra Musa amesema, idadi jumla ya watu waliokufa itatolewa baada ya zoezi la uokozi kufungwa.

Amesema hadi sasa miili 27 imepatikana kufuatia ajali hiyo iliyotokea siku ya Alhamisi usiku na kazi ya kuwasaka wahanga inaendelea.

Boti hiyo kwa kiasi kikubwa ilikuwa imewabeba wafanyabishara wa jamii ya Missa, jimbo la Kogi waliokuwa wakielekea kwenye soko la wiki katika  jimbo jirani la Niger na hawakuwa wamevaa vifaa vya kujiokoa, hali iliyosababisha wengi kuzama majini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW