1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Karibu watu 80 watekwa nchini Nigeria

8 Aprili 2023

Genge la watu wenye silaha limewateka nyara wanakijiji wasiopungua 80 wengi waowanawake na watoto katika jimbo la Zamfara, Kaskazini Magharibi mwa Nigeria.

Nigeria Rigasa | Polizist am Bahnhof an der Abuja-Kaduna Zugstrecke
Picha: Olukayode Jaiyeola/NurPhoto/picture alliance

Eneo hilo linafahamika kuwa kitovu cha utekaji nyara unaofanywa na makundi ya kihalifu yakivilenga vijiji kwa malengo ya kupata fedha ya kikomboleo.

Soma Zaidi: Watoto kadhaa watekwa nyara katika jimbo la Katsina, Nigeria

Duru zinasema mkasa huo wa hivi karibuni kabisa umetokea jana Ijumaa katika kiji cha Tsafe ambapo genge la wata liliwakamata kwa nguvu watoto na wanawake waliokuwa wakilima na wengine wakitafuta kuni kwenye msitu ulio jirani na kijiji.

Polisi ya jimbo la Zamfara limethibitisha kisa hicho lakini haikutaja idadi kamili ya watu waliotekwa nyara na imearifu kwamba inafanya kazi na jeshi kuwatafuta na kuwaokoa watu hao.