1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Watu 94 wafa nchini Msumbiji baada ya boti kupinduka

8 Aprili 2024

Karibu watu 96 wamekufa na wengine 26 wakiwa hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa imepakia abiria 130 kupinduka kaskazini mwa Msumbiji.

Mosambik Pemba | Geflüchtete Menschen | Paquitequete Strand
Picha: DW

Afisa kutoka taasisi ya Usafiri wa Majini, INTRASMAR Lourenco Machado amesema kupitia kituo cha televisheni ya taifa kwamba boti hiyo ya uvuvi ilikuwa imejaza abiria kupita kiasi na licha ya kwamba haikuwa na kibali cha kubeba abiria.  

Amesema wamefanikiwa kupata miili 94 na 26 bado hawajapatikana.

Boti hiyo ilikuwa ikiwavusha watu kutoka Lunga katika jimbo la Nampula na kuwapeleka kwenye Kisiwa cha Msumbiji na kuongeza kuwa huenda ilipigwa na dharuba kali.

Abiria hao walikuwa wakimkimbia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, hii ikiwa ni kulingana na kituo cha utangazaji cha serikali, TVM, kilichomnukuu afisa wa usafiri wa majini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW