Karzai ailaumu Pakistan
4 Desemba 2011Matangazo
Karzai ameliambia jarida la habari la Spiegel kuwa Pakistan , ambayo inasusia mkutano huo, imekataa kuunga mkono juhudi za majadiliano na Taliban.
Mkutano wa Bonn unataka kutafuta mwelekeo kwa Afghanistan baada ya kujitoa kwa majeshi ya NATO, lakini ususiaji wa Pakistan umeleta pigo kwa mwelekeo kama huo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle pia amesikitishwa na uamuzi wa Pakistan, akisema kuwa nchi hiyo itafaidika zaidi kutokana na amani nchini Afghanistan kuliko nchi jirani nyingine yoyote. Wakati huo huo , mjini Bonn jana , maelfu ya watu waliandamana mitaani kuupinga mkutano huo pamoja na jukumu la Ujerumani nchini Afghanistan.