KASHFA YA KABUMBU UJERUMANI
4 Februari 2005Wakati akihudhuria tafrija moja hapo Juni 1971, mwanabiashara Horst Gregorio Canellas, aliyekuwa Rais wa Kilabu ya Kabumbu Kicker Offenbach alifichua siri ya kuweko mtandao mzima wa harakati za usaliti katika Ligi ya kwanza ya Ujerumani. Muda si muda iliporomoka kama nyumba ya karata ile imani ambayo watu walikuwa nayo katika vilabu vya kabumbu. Dukuduku la ukumbusho huo limerudi tena sasa wakati kashfa za wakati kabumbu la Ujerumani zikizidi kugonga vichwa vya habari. Mwaka 1971 ilijitokeza kiöuvu tu cha kile ambacho sasa mtoa mashtaka mkuu wa serikali amekita kwa Kijerumani: "Ncha tu kileleni mwa mlima wa barafu", Wahusika wa wakati huo walichafua sifa yao walipokula rushwa hafifu, na kashfa zao zisimawe wapi mbele ya kipimo cha ukurasa wa kashfa za sasa uliofunguliwa na Robert Hoyzer. Mwanzo mwanzo Shirika la Kabumbu la Ujerumani lilifanya kana kwamba kashfa hiyo ilikuwa kashfa mwamuzi mmoja binafsi. Lakini baada ya kufanya taftishi na operesheni za kuvamia nyumba za washutumiwa, siku baada ya siku taasisi za kisheria za kiserikali zinazidi kuthibitikiwa na ukweli kuwa kisa cha Hoyzer kilikuwa ni mwanzo tu wa mtandao wa kijambazi na kihalifu yanayoyaingiza magengi ya kimafia. Zamani inajulikana namna rushwa na michezo ya kamari inavyoweza kuathiri matokeo ya mashindano ya farasi. Na ikiwa zitakuja thibitika shutuma basi matokeo ya mchezo ya aina mbali mbali itakabiliwa na kitisho cha kushawishiwa na ulaji rushwa na siyo peke yake Ujerumani bali duniani kote. Mpaka hivi sasa sekta ya michezo imeweza kujikinga na kashfa kama hizo kwa sababu mahakama ya michezo ikiwapa adhabu kali wenye hatia. Lakini kwa kuwa sasa umehusika ujambazi wa hali ya juu na matokeo ya michezo kuweza kuwaumiza wanariadha na wachezaji wenyewe kwa sababu na kiuchumi nao washabiki wa michezo kuweza kudanganywa bila ya wao kujua nini kinachotokea nyuma ya mapazia, linazidi kuulizwa swali iwapo unatosheleza mfumo wa sasa wa sheria za kupambana na uhalifu kama huo?
Zamani Ufaransa imechukua hatua muwafaka baada ya waendesha baisikeli wa mashindano ya Tour de France kuzusha kashfa ya kula madawa ya kutia nguvu. Baada ya kudhihirika kashfa za wakimbiaji wa Kigiriki wa masafa mafupi wa Kigiriki Kenteris na Thanou muda mfupi kabla ya kuanza michezo ya Olympic mjini Athens mabingwa wengi wanayochunguza madawa ya kutia nguvu hawazungumzi tena juu ya kuhussika wasaliti wadogo wadogo katika michezo bali juu ya mitandao mikubwa mikubwa ya wajambazi wa michezo.