1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kashfa ya waziri wa afya ulla Schmidt

28 Julai 2009

Uchambuzi pia uligusia mapatano ya kumaliza mgomo wa Kindergarten.

Gari la Bibi Ulla SchmidtPicha: picture-alliance/ dpa

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo yametuwama juu ya kashfa ya waziri wa afya wa Ujerumani bibi Ulla Schmidt inayohusika na kutumia gari la kifahari la serikali

kwenda Spain eti kwa shughuli 2 za kiserikali.Mada nyengine ni maafikiano kati ya nchi za Umoja wa ulaya kupeana taarifa za kibenki juu ya watu wanaoshjukiwa.Maafikiano ya kumaliza mgomo wa kindergarten pia yamechambuliwa:

Kuhusu mkasa wa waziri wa afya bibi Ulla Schmidt, gazeti la Westfalische Zeitung kutoka Bielefeld laandika:

"Miadi 2 za kipumbavu ambazo waziri huyo akihisi hata hajastahili kuzitaja, ndizo zilizopolekea yeye kutumia gari la kifahari kufunga safari hadi Spain.Lakini tatizo gani la usalama wake mbali na kuungua ngozi ya mwili wake kwa jua kali la Costa Bianca,uliopelekea kubidi kutumia gari hilo ?

Kisheria ,yamkini hakuna la kuhoji safari hiyo,hatahivyo, amewatia viongozi wenzake wa chama kinacho yumbayumba wakati huu katika mashaka yasiohitajika.Kuwa mwanasiasa mzuri sio tu ni kuonesha matokeo mema bali pia kupima athari ya anayofanya."

Gazeti la Pforzheimer Zeitung likichambua zaidi kisa cha bibi Schmidt, lauliza :kisa cha bibi Schmidt kitakua na athari gani ?

Linajibu kuwa hakitakua na athari zozote......Tatizo hapa ni kuwa mikasa kama hii ya Bibi Schmidt ya kutumia gari la serikali kibinafsi,huwezi kuuzuwia kutokea tena.Kwani kuna mwanya kati ya kulitumia gari la serikali kwa shughuli zinazoruhusiwa yapasa kutumika busara iwapo kuna haja kama hiyo.

Kwa maoni ya gazeti la Nordbayerrischer Kurier, safari ya Bibi Ulla Schmidt huko Spain akipanda motokaa ya serikali, ni mada inayojaza pengo la kipindi hiki cha likizo kwa upinzani bungeni ingawa ni mkasa usiotosha kujaza pengo hilo. gazeti laongeza:

Safari ndogo huko pwani ya Spain ya Costa Blanca hatahivyo inatilia nguvu maoni ya wengi yaliopo kuwa wanasiasa wanatumia vibaya madaraka yao. Kwa shughuli za kibinafsi.

...Mapokezi kwa meya wa jiji hilo la Spain na je,kutoa hotuba kilomita 8 kutoka kituo cha kitalii cha mapumziko,kunastahiki gharama yote hiyo-lauliza gazeti?

Kubana matumizi ya serikali kunaanzia mambo madogo madogo,lasema gazeti.Bibi Ulla Schmitd katika kipindi hiki cha msukosuko wa uchumi,ametoa ishara isiopendeza-lasema Nordbayerische Zeitung.

Likitugeuzia mada ,gazeti la BADISCHE ZEITUNG huko Freiburg lazungumzia mpango ulioafikiwa wa kupeana taarifa za shughuli za kibenki miongoni mwa nchi zanachama wa Umoja wa Ulaya na Marekani. Gazeti laandika:

"Magaidi wengi kitambo sasa walikwisha gundua njia nyengine za kusafirisha fedha kwa njia za chini kwa chini.Wachunguzi wengi wanahisi kuwa, dai la Marekani kuzichunguza taarifa hizo za kibenki, zaidi ni kufanya ujasusi wa kiuchumi kuliko kupiga vita ugaidi.

Kwani, kupitia mfumo wa SWIFT,Marekani inaweza kuzikagua nyendo zote za fedha za mabenki yote madogo-madogo na hata makampuni.

Idara ya ujasusi ya china haitaachiwa kuaminiwa kutupa macho yaked katika shughuli za kibenki za nchi hizo.Serikali ya Ujerumani kwahivyo inapaswa kuchunga kabla ya kufufunga mapatano hayo na Marekamni itafafanue wazi kufanya hivyo kunaleta manuifaa gani.

Mwishoe, gazeti la Kolnische Rundschau linayachambua mapatano ya kumaliza mgomo wa shule za chekechea au kindergarten.Linasema maafikiano yaliofikiwa ni habari njema.

Laongeza:

"Iwapo makubaliano hayo yataleta faida yoyote na yataweza kugharimiwa ni swali linaloweza kujibiwa tu na wale waliotia saini kuyaidhinisha."

Muandishi: Ramadhan Ali/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman