Kasisi achomwa kisu Uturuki
17 Desemba 2007Matangazo
IZMIR
Kasisi wa Kikatoliki amechomwa kisu katika mji wa magharibi mwa Uturuki wa Izmir.
Polisi imesema kasisi huyo Adriane Francini ameshambuliwa kwenye kanisa la St. Antoine lakini maisha yake hayako hatarini.Shirika la habari la Anatolia limeripoti kwamba mashambuliaji mwenye umri wa miaka 19 alikamatwa muda mfupi baadae.Mtuhumiwa huyo ameiambia polisi kwamba aliwasiliana na kanisa hilo kutokana na udadisi na kwamba kanisa lilimkaribisha ahudhurie misa.
Hili ni shambulio jipya katika mfululizo wa mashambulio dhidi ya Wakristo nchini Uturuki nchi ya Kiislam ambayo inajivunia kwa msimao wake wa kutoegemea dini yoyote ile.