KATHMANDU Marekani yaionya Nepal.
18 Februari 2005Marekani imetoa onyo kali kwa mfalme wa Nepal, Gyanendra, aliyenyakua madaraka majuma mawili yaliyopita, kurudisha maongozi ya kisheria nchini humo. Balozi wa Marekani, James Moriarty, amesema Marekani, mataifa ya Ulaya na India, ambazo juma hili ziliwaondoa wajumbe wao kutoka Nepal, zitafikiria kufutilia mbali misaada ya kijeshi kwa taifa hilo. Gyanaendra anasema alinyakua madararaka ya kuiongoza Nepal kukabiliana barabara na wapiganaji wa Mao. Wanasiasa wa Nepal wanasema mamia ya wanachama wao, vyama vya wafanyakazi, makundi ya kutetea haki za binadamu na makundi ya wanafunzi wametiwa mbaroni na kuwekwa katika vifungo vya nyumbani. Vyombo vya habari vya kitaifa vimetangaza kwamba waasi 43 wa mao wameuwawa katika mapigano kati yao na walinda usalama wa kitaifa.
