1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KATHMANDU: Raia washerehekea mkataba wa amani

23 Novemba 2006

Nchi ya Nepal imekuwa katika sherehe kutokana na kusainiwa mkataba wa amani kati ya serikali na waasi wa Maoist. Maelfu ya raia wamejitokeza barabarani katika mji mkuu Kathmandu na miji mingine kusherehekea mkataba huo ambao umemaliza vita vya mwongo mzima ambapo watu 13,000 waliuawa.

Kulingana na mapatano hayo, waasi wa Maoist ambao walipigania kuuondoa ufalme, watajiunga na serikali ya mpito na silaha zao zitakuwa chini ya udhibiti wa Umoja wa mataifa. Uchaguzi wa bunge umepangwa kufanyika mapema mwaka ujao.