1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu Mkuu wa CAF Veron Mossengo ajiuzulu

Saleh Mwanamilongo
29 Machi 2026

Veron Mossengo-Omba, mwenye umri wa miaka 66, na raia wa Kongo, amesema anaacha kazi ili kujihusisha na miradi yake binafsi, lakini anatarajiwa.

Katibu Mkuu wa CAF Veron Mossengo-Omba ( kushoto) ajiuzulu huku soka la Afrika likikabiliwa na ukosoaji
Katibu Mkuu wa CAF Veron Mossengo-Omba ( kushoto) ajiuzulu huku soka la Afrika likikabiliwa na ukosoajiPicha: Weam Mostafa/Sports Inc/empics/picture alliance

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, Veron Mossengo-Omba, amejiuzulu wadhifa wake huo Jumapili (Machi 29,2026).

Uamuzi huu unakuja wakati CAF inakabiliwa na ukosoaji mkubwa baada ya kuondolewa taji la Kombe la Afrika kutoka Senegal na madai ya ufisadi ndani chombo hicho cha kandanda barani Afrika.

Mossengo-Omba, mwenye umri wa miaka 66, amesema anaacha kazi ili kujihusisha na miradi yake binafsi, lakini anatarajiwa kugombea urais wa shirikisho la soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, FECOFA. Hatua hii inafuatia changamoto kubwa kwa uongozi wa CAF na mashaka kuhusu uadilifu wa mashindano ya soka barani Afrika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW