Katibu Mkuu UN ahimiza juhudi mpya kukomesha ghasia DRC
6 Mei 2023Guterres aliuambia mkutano ngazi ya juu uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi uliowahusisha marais na viongozi wengine wakuu wa mataifa ya Afrika ambayo yametia saini makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2013 kwa ajili ya kuendeleza utulivu na usalama nchini Kongo.
Soma zaidi:UN: Zaidi ya raia 1,300 wameuawa katika machafuko, DRC
Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema makubaliano yaliyoanzishwa muongo mmoja uliopita yanaashiria mabadiliko ya ushirikiano katika taifa hilo lenye utajiri wa madini linalokumbwa na migogoro. Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa ametanabahisha kwamba licha ya juhudi za pamoja, zaidi ya makundi 100 yanayomiliki silaha ndani na nje ya Kongo bado yanatishia uthabiti wa eneo zima la Maziwa Makuu. Amesisitiza kwamba mazungumzo ya dhati ya mara kwa mara ndiyo njia pekee ya kuleta maelewano na amani ya kudumu katika eneo hilo.