1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu mkuu wa FIFA Fatma Samoura kuachia ngazi

15 Juni 2023

Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni-FIFA limetangaza kuondoka kwa Katibu Mkuu wake Fatma Samoura, baada ya kuhudumu kwa takribani miaka saba.

FIFA | Gianni Infantino und Fatma Samba Diouf Samoura
Picha: Ulmer/IMAGO

Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni-FIFA limetangaza kuondoka kwa Katibu Mkuu wake Fatma Samoura, baada ya kuhudumu kwa takribani miaka saba.

Hata hivyo FIFA imesema Samoura atasalia katika kazi anayoifanya tangu 2016 katika kipindi cha Kombe la Dunia la Wanawake la mwaka huu litakalofanyika huko Australia na New Zealand na kuondoka kabisa mwishoni mwa mwaka.

Soma kuhusu: Gianni Infantino achaguliwa tena rais wa FIFA

Afisa huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa mwenye umri wa miaka 60 kutoka Senegal aliukwaa wadhfa usiotarajiwa miaka saba iliyopita mara tu baada ya kuchaguliwa kwa Gianni Infantino kama rais wa FIFA.

Amekuwa mwanamke wa kwanza, mtu wa kwanza Mweusi, wa kwanza Mwislamu na wa kwanza asiye mzungu kuwa katika mamlaka ya juu ya usimamizi wa FIFA.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW