1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Stoltenberg ataja mafanikio ya Ukraine katika uwanja wa vita

29 Septemba 2023

Katibu Mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amekutana na Rais Volodymyr Zelensky mjini Kiev wakati wa ziara yake ya pili nchini Ukraine tangu uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka jana.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg (kushoto) akisalimiana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Kiev
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg (kushoto) akisalimiana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini KievPicha: Ukrainian Presidential Press Office/AP Photo/picture alliance

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Stoltenberg amesema wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kupata mafanikio katika uwanja wa mapambano dhidi ya "wavamizi wa Urusi."

Katibu Mkuu huyo wa NATO ameeleza kuwa, Waukraine wanapigania familia, mustakabali na uhuru wao tofauti na Urusi inayolenga tu kupanua mamlaka yake.

Zelensky ametangaza hati mpya ya pamoja inayoweka bayana hatua za kinadharia kwa Ukraine kufikia viwango vya NATO.

Kwa miezi kadhaa sasa, serikali ya Kiev imekuwa ikishinikiza kupewa uwanachama kamili wa NATO na Umoja wa Ulaya pindi tu vita vyake dhidi ya Urusi vitakapokwisha.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW