Stoltenberg: Bajeti ya kijeshi imeongezeka kwa 11%
14 Februari 2024Matangazo
Stoltenberg amesema anatarajia wanachama 18 watatenga asilimia 2 ya mapato jumla ya nchi zao hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Katibu Mkuu wa mfungamano wa kijeshi wa NATO ameeleza kuwa hilo ni ongezeko la mara sita zaidi kuliko ilivyokuwa mnamo mwaka 2014 ambapo ni nchi tatu tu wanachama zilizofikia kiwango hicho.
Soma pia:Ujerumani yafikia lengo la NATO katika kujilinda
Mnamo mwaka 2006 nchi wanachama wa NATO zilikubaliana kutenga asilimia 2 ya pato jumla kwa ajili ya ulinzi lakini ni nchi chache tu zilizofikia lengo hilo.