1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

NATO yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine

21 Juni 2023

Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO, Jens Stoltenberg ameahidi kutoa ahadi nyingine katika mkutano wa kilele wa taasisi hiyo mwezi ujao,ya kusaidia kulijenga jeshi la Ukraine kuwa la kisasa.

USA NATO Generalsekretär Jens Stoltenberg in Washington
Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Katika matamshi yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Ujerumani la Tagesspiegel leo Jumatano, Stoltenberg amesema washirika wa NATO watapitisha msaada mkubwa katika mkutano wa Vilnius, ambao utaisaidia  Ukraine kufikia viwango vya NATO.

Kadhalika ametilia mkazo umuhimu wa kuendelea kuisaidia nchi hiyo ambayo imekuwa ikipambana na Urusi tangu uvamizi wa Februari mwaka 2022.