Katibu Mkuu wa NATO kukutana na Trump mjini Washington
8 Aprili 2026
Matangazo
Trump ambaye amekuwa akiwatuhumu washirika wa Ulaya kwa kushindwa kusaidia kuufungua Mlango-Bahari wa Hormuz uliofungwa kutokana na vita vya Iran, ametishia mara kadhaa kuiondoa Marekani kwenye jumuiya ya NATO.
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kuzungumza kuhusu mzozo wa Ukraine na Mashariki ya Kati. Ikulu ya White House imesema mkutano huo umepangwa kufanyika faraghani lakini huenda hilo likabadilika mnamo dakika za mwisho na hivyo kuwaruhusu waandishi wa habari kuhudhuria.