1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mark Rutte azitaka nchi wanachama kuisaidia Ukraine

3 Desemba 2024

Katibu mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Mark Rutte ameyatolea mwito mataifa wanachama kujielekeza zaidi katika kuihami Ukraine kwa silaha kuliko kujadili kinachoweza kutokea kumaliza vita vinavyoendelea.

Mark Rutte
Katibu mkuu wa NATO Mark RuttePicha: François WALSCHAERTS/AFP

 

Rutte amesema Ukraine haihitaji kupewa mawazo zaidi kuhusu namna mchakato wa amani unavyoweza kufanyika, bali inahitaji nguvu za kijeshi.

''Lakini tutahitaji kuchukuwa hatua zaidi na hasahasa wakati huu. Kadri uungaji mkono wetu kijeshi utakavyokuwa kwa Ukraine hivi sasa ndivyo nchi hiyo itakavyokuwa na sauti katika meza ya mazungumzo na ndivyo tutakavyomaliza kabisa uchokozi wa Urusi haraka nchini Ukraine,'' alisema Rutte.

Antony Blinken na Rutte wa NATO wakutana kuhusu vita Ukraine

Kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa NATO mjini Brussels, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Andriy Sybiga alitowa mwito kwa nchi za jumuiya hiyo kuipelekea alau mifumo 20 zaidi ya ulinzi wa anga kuzuia mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundo mbinu yake ya nishati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW