1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katibu Mkuu wa NATO kufanya ziara ya siku mbili Marekani

13 Julai 2025

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte atafanya ziara ya siku mbili mjini Washington. Rutte atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth.

Rutte atakutana na kufanya mazungumzo na Donald Trump mjini Washington
Katibu Mkuu wa NATO Mark RuttePicha: Matthias Schrader/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa kupitia taarifa iliyotolewa Jumapili japo haikufafanua madhumuni ya ziara ya Rutte itakayoanza Jumatatu 14.07.2025 nchini Marekani. Hata hiyo hivi karibuni Trump alisema katika mahojiano na kituo cha habari cha NBC kwamba Marekani itakuwa tayari kuipatia silaha Ukraine kupitia Jumuiya ya kujihami ya NATO na kwamba angelitoa "taarifa muhimu" kuhusu Urusi Jumatatu.

Utawala wa Trump umekuwa ukituma silaha zilizoidhinishwa na mtangulizi wake Joe Biden, aliyeiunga mkono kikamilifu Kyiv. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa akiwatolewa wito washirika wake wa Magharibi kuipatia silaha zaidi ili kukabiliana na mashambulizi ya Urusi yanayoongezeka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW