1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KATIKA MICHEZO YA OLIMPIK YA ATHENS, AFRIKA KUSINI YAIPATIA AFRIKA MEDALI YAKE YA KWANZA YA DHAHABU.IRAK YAINGIA KAMA ARGENTINA DURU IJAYO YA ROBO-FINALI YA DIMBA LA OLIMPIK

Ramadhan Ali16 Agosti 2004

OLIMPIK ATHENS:

Baada ya mstuko na msangao wa jana katika viwanja vya olimpik ambamo Afrika kusini ilimvunjia Muamerika Michael Phelps ndoto yake ya kutwaa medali 8 za dhahabu kutoka hodhi la kuogolea;pigo kwa timu ya mpira wa kikapu ya Mirak ikikata tiketi yake ya robo-finali ya dimba la olimpik kwa ushindi mwengine maridadi dh siku ya 4 ya michezo hii kutoka hodhi la kuogolea;Gymnastics, vyuma vizito-weightlifting, kutunga shabaha-shooting hadi judo-miereka.

Wanariadha 4 wa Afrika Kusin, walinyakua medali ya kwanza ya dhahabu kwa bara la Afrika katika michezo ya 28 ya olimpik,athens.Medali hiyo, ilikua katika hodhi la kuogolea katika mita 100X4 kupokezana -freestyle.Kwa ushindi huo wa rekodi ya dunia ya dakika 3,sekunde 13.17,wanariadha Roland Schoeman,Lyndon Ferns,Darian Townsend na Ryk Neethling walimtilia kitumbua chake mchanga bingwa wa marekani Michael Phelps aliepigiwa upatu na kuhanikiza angelitwaa medali 8 za dhahabu kutoka michezo hii ya kuogolea na hivyo kumpik Mark Spitz wa marekani alienyakua medali 7 za dhahabu katika michezo ya Olimpik ya Munich,1972.

Ushindi wa waafrika Kusini hao ulipokewa kwa shangwe na shamra shamra huko Johannesberg na miji mengine ya Afrika Kusini.

Katika medani ya riadha itakayoanza kutia fora ijumaa ijayo, wanariadha 2 wa Ugiriki, wangali wakigonga vichwa vya habari baada ya leo hii kushindwa tena kufika mbele ya Kamati ya nidhamu ya IOC-halmashauri kuu ya Olimpik ulimwenguni kuhusu kisa chao cha kukwepa uchunguzi wa madhambi ya doping-matumizi ya madawa kuongezea kasi.

Wao ni bingwa wa olimpik wa mita 200 Kostadinos Kenteris na mshindi wa medali ya fedha wanawake Ekterini Thanou.Wote wawili waliwakilishwa leo na kocha wao Christos Tzekos na wakili wao Michalis Dimitrakopoulos,waliothibitisha kuwa wanariadha hao hawangehudhuria kikao cha loe.Tume ya IOC ikitazamiwa jioni ya leo kukutana kuamua hatima ya wanariadha hao iwapo kuwafukuza wasishiriki katika mic hezo hii ya Athens au la.

Bingwa wa zamani wa dunia na Olimpik wa Ethiopia katika masafa ya mita 10.000 , mzee Mirus Yifter ,ameabashiri kwamba, chipukizi wa Ethiopia ,Kenenisa Bekele ataibuka bingwa tangu katika masafa ya mita 5000 hata 10,000.hasimu yake mkubwa katika mita 10,000 atakua bingwa wa mabingwa Haile Gebre-selasie pia wa Ethiopia.

Na taarifa kutoka Athesn, zasema leo bingwa mwengine wa mita 10,000 wa dunia wa Ethiopia upande wa wanawake-Berhane Adere ameondolewa katika orodha ya wale watakaokimbia mbio hizo mjini Athesn,kwavile aonesha ameumia na akifanya mazowezi kwa shida.

Shirikisho la riadha la Ethiopia limearifu kuwa, mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 31,nafasi yake sasa itachukuliwa na bingwa wa michezo ya bara la Afrika:all-Africa Champions Ejegayehu Dibaba.Dibaba mwenye umri wa miaka 22 alipanga kukimbia masafa ya mita 5000,lakini alikataa kujaribu masafa yote 2: 5000 na 10,000.Nafasi yake sasa katika mita 5000 itachukuliwa na Meseret Defar, bingwa wa dunia wa mashindano ya ukumbini ya masafa 3,000.

Maafisa wa mchezo wa miereka-judo wamearifu leo wanahitaji kukusanya ushahidi zaidi kabla kuchukua hatua yoyote dhidi ya Iran kwa kufanya mgomo unaobainika kama wa kisiasa katika michezo hii ya Olimpik:Bingwa wake wa dunia Arash Miresmaeli alipangwa kupambana na Ehud Vaks wa Israel katika duru ya kwanza ya changamoto ya chini ya kilo 66 jana ,lakini aligunduliwa amevuka uzito wa daraja hiyo.baadae,Miresmaeli alinukuliwa kusema alikwepa kupigana na Muisraeli huyo kwa kuwahurumia wapalestina.Msemaji nchini Iran aliarifu kwamba, Miresmaeili alitakiwa kujitoa mashindanoni kulingana na sera za Iran kuelekea Israel.

Risasi zilifyatuliwa jana usiku mjini Baghdad na hii lakini si ajabu wakati huu wa vita.

Maajabu lakini kwa kuwa zililengwa angani kushangiria ushindi mwengine wa timu yao ya dimba ya Olimpik.Iraq jana iliizaba costa rica mabao 2-0 na hivyo imeshakata tiketi yake ya robo-finali.

Argentina ambayo nayo tayari imeshqaingia robo-finali inacheza jioni hii na australia,wakati Korea ya kusini inachuana na Mali,ambayo iliwashinda wenyeji Ugiriki 2:0 katika mpambano wao uliopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW