1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Katika Soka: Brazil mabingwa wa Confederation Cup.

30 Juni 2005

Brazil imeshinda kombe la Confederation baada ya kuwaswaga Argentina kwa mabao 4-1 katika fainali mjini Frankfurt.

Mshambuliaji wa Brazil Adriano alifunga mabao mawili katika mchezo huo wa fainali na kutimiza mabao matano ambayo yamempa tuzo ya kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora katika mashindano hayo.

Pia ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.

Ujerumani iliishinda Mexico na kushika nafasi ya tatu katika mchezo mwingine jana uliofanyika Leipzig.

Nahodha ya Ujerumani Michael Ballack aliipatia timu yake bao la ushindi kwa mkwaju wa adhabu mita 40 kutoka golini katika kipindi cha nyongeza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW