Katz: Tutawamaliza Hamas wasiporidhia masharti ya vita
22 Agosti 2025
Matangazo
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa X, Katz alisema “milango ya jehanamu” itafunguliwa dhidi ya Hamas, ambao aliwaita wauaji, hadi watakapokubali masharti ya Israel ya kumaliza vita.
Ameonya kuwa iwapo kundi hilo la Kipalestina halitakubaliana na masharti hayo, Gaza itageuzwa kuwa mfano wa Rafah na Beit Hanoun, maeneo yaliyosambaratishwa vibaya kufuatia mashambulizi ya Israel.
Asilimia 83 ya waliouwawa Gaza ni raia
Matamshi haya yamejiri baada ya mkutano wa usalama uliofanyika jana, ukihudhuriwa na Netanyahu na maafisa wa juu wa kijeshi, ambapo operesheni ya kuudhibiti mji huo upande wa kaskazini iliidhinishwa rasmi.
Mpango huo pia unahusisha kuwaondoa zaidi ya watu milioni moja wanaoishi katika Ukanda wa Gaza.