Kaya 15 zachwa bila makao katika eneo la 58 mjini Nakuru
19 Aprili 2023Waathiriwa walishtuliwa na milio ya tingatinga mchana wa leo na wanalalamika kuwa hawana pa kwenda wala hawajui watawapeleka wapi watoto wao.
Ardhi hiyo ina kesi mahakamani ambapo wakaazi wanalalamika kwamba ilikuwa imekodishwa kwa njia isiyo halali na hakuna namna serikali ingedai kwamba inawafurusha ili ijenge nyumba za bei nafuu.
Maafisa wakuu wa usalama serikalini walikuwepo kusimamia zoezi hilo, lakini hawakutaka kunukuliwa.
Eneo la Nakuru limeshuhudia matukio mengi ya watu kufurushwa kwenye ardhi zao. Mwezi Februari mwaka huu familia 105 zilifurushwa eneo la Rongai, hatua iliyosababisha Naibu Rais Rigathi Gachagua kuingilia kati.
Katibu msimamizi katika wizara ya ardhi, Kimani Ngunjiri pia anachunguzwa na polisi kufuatia jaribio la kumpiga risasi mwanamke mmoja mzee kutokana na mzozo wa ardhi.