JamiiUganda
Kaya 5,000 zahamishwa kutoka eneo la maporomoko Uganda
16 Desemba 2024Matangazo
Maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa mwishoni mwa mwezi Novemba yalisababisha vifo vya karibu watu 36 katika wilaya ya Bulambuli, huku makumi ya wengine wakihofiwa kufariki baada ya kufunikwa na tope.
Soma pia: Vifo vya maporomoko ya udongo Uganda vyafikia 28
Tangu wakati huo serikali imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea janga jingine baada ya ufa mkubwa kuonekana ardhini. Wilaya zinazohusika na agizo hilo ni Bulambuli, Mbale, Sironko, Kapchorwa, Kween, Bukwo na Bududa.
Serikali ya Uganda imetoa muda wa wiki mbili kwa wakaazi kuhama kabla ya mamlaka kuingilia kati na kuwalazimisha kuondoka na kusisitiza kuwa wote watakaohamishwa watapewa msaada wa pesa na makazi mapya.