1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKazakhstan

Kazakhstan yataifisha kampuni baada ya mkasa wa moto mgodini

28 Oktoba 2023

Kazakhstan leo imeitafisha kampuni moja kubwa ya kuchimba madini saa chache baada watu 32 kupoteza maisha kwenye mkasa wa moto uliotokea katika moja ya migodi ya kuchimba chuma inayomilikiwa na kampuni hiyo.

Moja ya migodi ya kampuni ya ArcelorMittal
Kampuni ya ArcelorMittal imelaumu kwa kupuuza kanuni za usalama kwenye migodi yake.Picha: Ruslan Pryanikov/AFP

Taarifa ya kutaifishwa kwa kampuni ya ArcelorMittal inayoendesha migodi kadhaa ya chuma, makaa ya mawe na vito vya thamani nchini Kazakhstan, imetolewa na upande wa serikali na kuthibitishwa na uongozi wa kampuni hiyo.

Inafuatia ukosoaji mkubwa kutoka kwa rais Kassym-Jomart Tokayev aliyeitaja kuwa kampuni "hatari" katika historia ya taifa hilo baada ya kutokea mfululizo wa matukio yaliyosababisha vifo kwenye migodi inayoisimamia.

Hadi sasa chanzo cha mkasa wa moto wa leo bado haikijafahamika, lakini maafisa wamesema mbali ya watu 32 waliopoteza maisha wengine 14 bado hawajulikani waliko na juhudi za kuwatafuta ndani ya shimo la mgodi zinaendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW