Kazi na mafunzo
12 Januari 2010Ni kazi gani inanifaa mimi? Baadhi ya nyakati kuchukua hatua hii ya kwanza sio rahisi kabisa. Maripota wetu wanazungumza na watu katika kazi mbali mbali ili kupata taarifa ambazo zitaweza kufanya uchukuaji wa uamuzi huu kuwa rahisi. Wamegundua iwapo kuna uwezekano wa kuishi kama wanamuziki na vipi maisha yanavyokuwa kwa meneja wa hoteli. Pia wanaripoti juu ya vipi mtu anaweza kuwa mwalimu ama mtaalamu wa mambo ya kompyuta.
Jinsi ya kufikia lengo
Katika mfululizo wa ripoti maalum, wasikilizaji wake watasikia maelezo juu ya elimu muhimu ya kupata kazi nzuri. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ pia kinawapasha habari juu ya kupata fedha kwa ajili ya elimu ya chuo kikuu, jinsi ya kushiriki katika usaili wa kazi na jinsi ya kujitayarisha kwa maisha mapya katika chuo kikuu ama masomo tu ya juu.
Maelezo na ucheshi
Pamoja na kuzungumza na watu kuhusu kazi zao, „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ pia ina vipindi vya burudani. Katika mchezo wa redio, tunamfuatilia msichana ambaye anaondoka kutoka kijijini na kwenda mjini ili kutafuta degirii katika kilimo. Wasikilizaji wake watajiunga naye wakati akijaribu kujiweka sawa na maisha ya mjini na changamoto za maisha na kazi chuoni.
„Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Kwa taarifa zaidi ama kusikiliza vipindi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.dw-world.de/lbe. „Deutsche Welle Learning by Ear – Noa bongo! Jenga maisha yako“ kinadhaminiwa na wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani.